FAHAMU JINSI YA KUANZA KUTIMIZA NDOTO YAKO HATA KAMA UNADHANI NI NGUMU
Kinachofanya
watu wafanikiwe ukiacha bahati ni swala la kujituma katika wayafanyayo.
Haitoshi tuu kuota na kutamani kuwa wa aina fulani, haitoshi tuu kuwa
na mipango na mikakati isiyo na utekelezaji.
Wengi
hupenda kuwa watu wa visingizio yaani kutoa sababu ya kwanini hawafanyi
watakiwayo kufanya au kwanini hawajawa vile wanavyotamani kuwa.
Mara nyingi sababu wazitoazo ni wazi kuwa hazitaji kwamba wao pia
wanahusika na hali waliyonayo. Mara nyingi visingizio ni watu wengine
kuwakwamisha, au mazingira.
Ukitaka mabadiliko siku
zote fikiria kwamba sawa pamoja na yote unayoyaona kuwa ni magumu, je
wewe kweli nini unaweza kufanya, hata kama ni kidogo.
Pengine tatizo ni namna
ya tabia yako ilivyo, pengine ni majivuno yako na kujiona wa thamani
zaidi au haufai kukabiliana na changamoto. Pengine ni kwakuwa haupo
tayari kusamehe, au kuendana na watu fulani ili mambo yaende sawa.
Pengine unahitaji ka uvumilivu kadogo tuu ili mambo yako yaende sawa.
Kanuni rahisi ya
kukumbuka katika kuwajibika na kuepukana kuwa mtu wa sababu ni kuamini
kuwa lengo lako ni la msingi zaidi kuliko hayo yanayokukwamisha. Anza
sasa kuweka mbele ndoto yako na usikubali mtu au mazingira yakufanye
urudi nyuma.
Usikubali watu-wasemayo
au tabia zao ziwe kikwazo cha ndoto yako kwani hayo ni mawazo yao,
kumbuka hata wewe una mawazo ambayo wengine hawawezi kuyabadilisha.
Usikubali kuweka mtazamo wa mtu mwingine mbele au unayodhani anawaza juu
yako mbele kuliko ndoto yako yenye thamani zaidi.
Kuhusu mazingira, kama
huwezi kubadili mazingira uliyopo basi vumilia na thaminisha kuwa ni
ndoto yako ni bora zaidi kuliko kuwa mnyonge wa mazingira. Ukifikira
zaidi utaona mazingira hayo magumu yanakupa fursa

0 comments:
Post a Comment